• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Marekani yamejenga daraja la Urafiki kwa wananchi wa nchi hizo

    (GMT+08:00) 2017-11-07 17:47:28

    Rais Donald Trump wa Marekani kesho ataanza ziara yake ya siku 3 ambayo ni ya kwanza hapa nchini China. Katika miaka ya hivi karibuni, China na Marekani zimeimarisha ushirikiano wao katika sekta ya utamaduni na mawasiliano kati ya watu, ambao umetoa nafasi kwa wananchi wa nchi hizo kuzidisha maelewano kati yao.

    Kuanzia tarehe 18 mwezi huu, jumba la sanaa la Virginia nchini Marekani litafanya maonyesho ya sanamu za askari na farasi wa enzi ya Qin katika historia ya China. Mkuu wa jumba hilo Alex Nyerges amesema China ni nchi pekee duniani yenye historia ya miaka elfu tano ambayo haijawahi kuvunjika, na ina vitu vingi vya kale visivyohesabika, na maonyesho kama hayo ni fursa nzuri katika kuonesha historia na utamaduni wa China kwa watu wa Marekani, pia ni muhimu kuhimiza uhusianowa nchi hizo mbili.

    "Wasanii wa kichina na utamaduni wa kichina vimetengeneza sanaa nzuri ya miaka elfu 5, lakini wamarekani wana ufahamu mdogo juu ya historia inayong'ara ya China, kwa hivyo kufanya maonyesho hayo hapa Virginia na kuonesha utamaduni wa kichina kwa wamarekani ni njia bora na jambo la kushangaza."

    Toka mwaka 2009, maonyesho 48 kama hayo yanayohusu China yamefanywa nchini Marekani, na kupata mwitikio mzuri wa kijamii. Naibu mkuu wa idara ya vitu vya kale vya kitamaduni ya taifa ya China Liu Shuguang amesema katika miaka ya hivi karibuni, China na Marekani zimewasiliana na kushirikiana katika sekta ya utamaduni kwenye ngazi mbalimbali.

    "Moja ni ushirikiano kati ya serikali. Mwaka 2009, China na Marekani zilisaini makubaliano yanayolenga kuimarisha ushirikiano kati yao katika kupambana na usafirishaji haramu wa vitu vya kale vya China nchini Marekani. Pili ni ushirikiano kati ya taasisi za kitaaluma. Tatu ni mawasiliano ya kitaaluma, ugunduzi wa vitu vya kale, maonyesho katika majumba na utoaji mafunzo."

    Uhai wa mawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Marekani umeongeza maelewano na urafiki kati ya wananchi wa nchi hizo mbili, na pia kuzidisha uhusiano wa aina mpya wa nchi kubwa kati ya China na Marekani. Bw. Liu Shuguang ameeleza kuwa katika siku zijazo, idara zinazoshughulikia utamaduni na majumba za nchi hizo zitavumbua hatua zao za ushirikiano, kupanua sekta zitakazofanyiwa ushirikiano na kufanya uhusiano wa kitamaduni kuwa sekta hai zaidi na yenye ubunifu katika uhusiano wa pande mbili kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako