• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waziarifu meli zilizoko katika eneo linalodhibitiwa na kundi la Houthi kuondoka mara moja

    (GMT+08:00) 2017-11-07 18:41:57

    Mfumo wa uthibitishaji na uangalizi wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen UNVIM umetoa taarifa ikiziarifu meli zote za kibiashara zilizoko katika eneo lililodhibitiwa na kundi la Houthi kuondoka mara moja.

    Taarifa imesema, kutokana na hali ya sasa ya usalama nchini Yemen, meli zote zikiwemo meli zilizotia nanga kwenye bandari ya bahari nyekundu zinatakiwa kuondoka mara moja, na kuelekea bandari au sehemu nyingine ili kuhakikisha usalama wa wanamaji, meli na mizigo.

    Taarifa pia imesema mfumo huo utasimamisha kwa muda kutoa vibali vya kwenda Yemen kwa meli, huku ikisisitiza kuwa hii ni hatua ya muda na utaendelea kufuatilia hali ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako