• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia ziara ya rais Trump nchini China itapata mafanikio ya kihistoria

    (GMT+08:00) 2017-11-07 18:48:59

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inatarajia ziara ya rais Donald Trump wa Marekani nchini China itapata mafanikio ya kihistoria, ili kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelezwa vizuri na kwa utulivu katika enzi mpya.

    Kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping wa China, kuanzia tarehe 8 hadi 10 mwezi huu rais Trump wa Marekani atafanya ziara nchini China. Hii itakuwa ziara ya kwanza ya kitaifa kwa China baada ya mkutano mkuu wa 19 wa chama cha CPC.

    Bi Hua amesema wakati hali ya kimataifa inapoendelea kubadilika, viongozi wa China na Marekani watakutana hapa Beijing kufanya tena mazungumzo ya kimkakati kuhusu masuala muhimu yanayofuatiliwa na pande mbili kwa lengo la kufikia makubaliano muhimu mapya baada ya viongozi hao wawili kukutana Marekani na Ujerumani, kuimarisha maelewano na urafiki na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano katika sekta mbalimbali. Ameongeza kuwa ziara hiyo itakuwa na maana kubwa katika kuendeleza kwa utulivu uhusiano kati ya pande mbili na kuhimiza amani, utulivu na ustawi wa sehemu ya Asia na Pasifiki na dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako