• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia kutoa dola milioni 600 kufadhili miradi ya miundo Afrika Mashariki na Kati

    (GMT+08:00) 2017-11-07 19:22:18

    Benki ya dunia inatarajiwa kutoa dola milioni 600 kufadhili miradi ya miundo mbinu ili kukuza biashara kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

    Katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki Liberat Mfumukeko amesema miradi hiyo itasaidia nchi za Burundi, Tanzania, Zambia na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

    Amesema hasa reli kwenye kanda hiyo itaimarisha usafirishaji wa biudhaa kutoka mjini Dar es Salaam hadi Kigoma, na baadaye kusafirishwa hadi Bujumbura, Kalemi na Uvira.

    Kulingana na jumuiya ya Afrika Mashariki, miradi hiyo itapunguza gharama za uchukuzi wa bidhaa kutoka bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 40.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako