• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Kahawa ya Uganda yatimiza viwango vilivyowekwa na soko la Sudan

    (GMT+08:00) 2017-11-07 19:23:51

    Kahawa ya Uganda imetimiza viwango vilivyowekwa na soko la Sudan ambayo ni soko lakep la pili kuu la bidhaa hiyo.

    Sudan ilikuwa imeipa Uganda muda wa miaka miwili bila masharti kutimiza viwango hivyo.

    Mkuu wa uratibu wa ubora kwenye kituo cha kukadiria ubora wa bidhaa nchini Uganda bwana Edmund Kananura Kyerere amesema maafisa wa idara ya ubora wa bidhaa kutoka Sudan pia wako nchini humo kwa muda wa wiki moja kutathmini mchakato wa kukuza na kupakia bidhaa hiyo.

    Naye naibu wa idara ya ubora wa bidhaa kutoka Sudan Zakaria Suliman Salih, amesema lengo lao ni kulinda wateja wa kahawa na pia kuhakikisha hakuna vizuizi vingi vya ukaguzi kwa bidhaa hiyo ya Uganda.

    Uganda huuza nje ya nchi kilo 800,000 nchini Sudan kila mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako