• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walihimiza eneo la Wakurd kuheshimu maamuzi ya mahakama kuu ya Iraq

    (GMT+08:00) 2017-11-08 08:58:43

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI imelihimiza eneo la Wakurd linalojitawala kuheshimu maamuzi ya mahakama kuu ya Iraq ambao umethibitisha umoja wa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na tume hiyo imenukuu taarifa iliyotolewa na msemaji wa mahakama kuu tarehe 6 baada ya mkutano wa mahakama, ikieleza wazi kwamba katiba inasisitiza umoja wa Iraq, na hakuna kifungu chochote kinachoruhusu eneo lolote kujitenga na Iraq.

    Tume hiyo imeihimiza serikali ya eneo la Wakurd kutambua, kuunga mkono na kuheshimu maamuzi ya mahakama kuu, na kusisitiza ahadi kamili ya kuheshimu katiba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako