• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa kiongozi wa chama cha ANC wapamba moto

    (GMT+08:00) 2017-11-08 09:11:46

    Kinyang'anyiro cha uchaguzi wa kiongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimepamba moto. Tawi la vijana la chama cha ANC kimejitokeza na kumkosoa Naibu Rais wa nchi hiyo Bw. Cyril Ramaphosa kwa kutangaza "timu ya ushindi" kuongoza chama tawala.

    Msemaji wa tawi la vijana Bw Mlondi Mkhize amesema kutangaza timu hiyo kunaonyesha kuwa Bw. Ramaphosa kutoheshimu mchakato wa chama na taratibu zake.

    Mwezi ujao chama cha ANC kitafanya uchaguzi wa mwenyekiti wake atakayechukua nafasi ya mwenyekiti wa sasa Bw. Jacob Zuma. Atakayechaguliwa kuwa mwenyekiti atakuwa na nafasi ya kuwa rais moja kwa moja, kama chama cha ANC kitashinda uchaguzi mkuu mwaka 2019.

    Tawi la vijana la chama cha ANC limeonyesha kuwa litamuunga mkono mwenyekiti wa tawi la wanawake wa chama cha ANC Bibi Nkosozana Dlamini Zuma kuwa mwenyekiti wa chama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako