• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa mataifa waanza kutoa huduma za afya kwenye vituo vya watu waliopoteza makazi yao nchini Sudan Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-08 09:12:12

    Shirika la uhamiaji la umoja wa mataifa IOM limekamilisha mpango wa kutoa huduma za afya kwenye vituo vitatu vya watu waliopoteza makazi yao nchini Sudan Kusini, kuwawezesha maelfu ya watu kupimwa, kupata ushauri nasaha, na tiba ya virusi vya ukimwi.

    Mpango huo utatekelezwa katika maeneo ya Bentiu, Malakal na Wau na kutarajiwa kuwanufaisha watu laki 1.7, ikiwa ni pamoja na wenyeji wa maeneo hayo.

    Umoja wa mataifa umesema mwaka jana idadi kubwa ya vifo vya watu katika vituo vyake vya kuwahifadhi watu waliopoteza makazi yao, ilitokana na virusi vya Ukimwi na kifua kikuu, na wengi wa watu hao hawakuweza kupata matibabu nje ya vituo hivyo. Kwa kupitia mfuko wa uungaji mkono wa duniani, IOM imetoa mafunzo kwa watu zaidi ya 450 kutoa ushauri nasaha nchini Sudan Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako