• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Misri asema hatabadilisha ukomo wa muda wa urais kwenye katiba

    (GMT+08:00) 2017-11-08 09:54:49

    Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri jana alipohojiwa na televisheni ya Marekani CNBC, alisema hatatafuta kubadilisha ukomo wa muda wa urais wa miaka minne kwa awamu mbili kwenye katiba, hali ambayo itamzuia kugombea urais kwa awamu ya tatu.

    Rais Sisi amesema uchaguzi mkuu wa Misri utafanyika mwezi Machi au Aprili mwaka kesho kama ilivyopangwa. Rais Al Sisi ametoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya wabunge kutaka kubadilishwa kwa kipengele cha katiba ili kumnufaisha.

    Rais Sisi hajatangaza rasmi kugombea awamu ya pili ya urais, lakini anatarajiwa kufanya hivyo na kupata ushindi mkubwa kutokana na hakuna wagombea wengine wenye nguvu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako