• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wafuatilia utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Yemen

    (GMT+08:00) 2017-11-08 10:02:55

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonesha wasiwasi juu ya mfululizo wa mashambulizi nchini Yemen yaliyotokea wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu wengi wakiwemo watoto.

    Msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu OCHA mjini Geneva Bw. Jens Laerke, amesema shughuli za kibinadamu zimekwama kutokana na kufungwa kwa viwanja vya ndege na bandari nchini humo.

    Kwa mujibu wa OCHA, ndege za kusafirisha misaada ya kibinadamu nchini Yemen zimekwama kuanzia Novemba, 6.

    Bw. Laerke anasisitiza kuwa vituo vyote vinahitaji kufunguliwa ili kuhakikisha chakula, nishati na dawa zinaweza kufikishwa nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako