• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 15 wa Taliban wauawa nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-11-08 10:05:29

    Wapiganaji 15 wa kundi la Taliban wameuawa katika mapambano na polisi baada ya kuvamia kituo cha kufanyia mazoezi cha polisi katika jimbo la Wardak nchini Afghanistan. Tukio hilo lililoanza kwa mpiganaji mmoja kutega bomu katika lango la kuingilia katika kituo hicho cha Dasht e Toap, lililolipuka na kuzusha mapigano kati ya polisi na wavamizi hao.

    Polisi wamethibitisha kutokea kwa vifo 15 vya wapiganaji wa Taliban waliokuwa pia wamevalia mabomu ya kujitoa mhanga.

    Tangu mwezi April mwaka huu wapiganaji wa kundi la Taliban wamekuwa wakifanya mashambulizi yaliyosababisha vifo na majeruhi nchini Afghanistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako