• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Korea Kusini na Marekani wasisitiza tena kanuni za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya amani

    (GMT+08:00) 2017-11-08 16:40:05
    Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amefanya mazungumzo na rais Donald Trump wa Marekani aliyekuwa ziarani nchini Korea Kusini, ambapo marais hao walisisitiza tena kanuni za kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea kwa njia ya amani na kuihimiza Korea Kaskazini kusimamisha mpango wa makombora ya nyuklia.
    Pande hizo mbili zimesema, kuendelea na silaha za nyuklia kwa Korea Kaskazini kutafanya nchi hiyo itengwe kidiplomasia na kuwa na hali ngumu kiuchumi. Kama nchi hiyo itaweza kutimiza hali isiyo na silaha za nyuklia kwa njia ya pande zote inayoweza kukaguliwa, na isiyoweza kurejesha hali ya zamani, peninsula ya Korea itapata amani ya kudumu.
    Habari nyingine zinasema, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesisitiza tena msimamo wa China kuhusu suala la nyuklia la Peninsuala ya Korea, akizitaka pande husika kufanya juhudi za pamoja kupunguza hali ya wasiwasi ya peninsula hiyo, na kurejesha suala hilo katika meza ya mazungumzo haraka iwezekanavyo.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako