• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lataka kuwepo kwa mpango wa jumla kupambana na uharamia kwenye pwani ya Somalia

    (GMT+08:00) 2017-11-08 16:49:09

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalolaani vitendo vya uharamia na uporaji katika pwani ya Somalia, na kutoa mwito wa kuwepo kwa mpango wa jumla wa kupambana na kutokomeza vitendo hivyo na kutatua vyanzo vyake..

    Azimio nambari 2383 la baraza la usalama linatambua wajibu wa msingi wa serikali ya Somalia kupambana na vitendo hivyo, na kuitaka serikali ya Somalia iendelee kuweka sheria za kupambana na uharamia na sheria za mambo ya bahari, na kuanzisha idara za usalama zenye majukumu ya wazi kwenye kusimamia sheria hizo.

    Azimio hilo pia limezitaka nchi zote wanachama wa umoja wa mataifa kuharamisha uharamia kwa kutumia sheria za ndani na kuwachukulia hatua maharamia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako