• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonyesho ya mawasiliano ya simu ya Afrika yafunguliwa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-08 16:49:40

    Maonyesho ya Mawasiliano ya Simu ya Afrika yamefunguliwa mjini Cape Town nchini Afrika Kusini, yakiwa na kauli mbiu ya kuimarisha mafungamano ya Afrika. Makampuni zaidi ya 400 ya sayansi na teknolojia na mawasiliano ya simu duniani, yakiwemo makampuni mengi ya China yataonyesha teknolojia na bidhaa zao mpya katika siku tatu zijazo.

    Maonyesho hayo yamefanywa kwa miaka 20 barani Afrika. Meneja mkuu wa Kampuni ya China Telecom tawi la Afrika Mashariki ya Kati Bw. Liu Changhai, amesema hayo ni maonyesho makubwa na yenye uwashiwi zaidi ya mawasiliano ya simu barani Afrika, ambapo si tu yanatoa fursa ya mawasiliano ya moja kwa moja kwa makampuni husika, bali pia ni dirisha la kujitangazia kwa makampuni yote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako