• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wajadili jinsi China na Marekani zitakavyofanya kutimiza mafanikio ya pamoja katika uchumi na biashara

    (GMT+08:00) 2017-11-08 16:55:09

    Rais Donald Trump wa Marekani leo ameanza rasmi ziara ya siku 3 nchini China, akiongoza ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara na wenye makampuni, ambao watashiriki kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi na kibiashara na kusaini makubaliano ya ushirikiano. Mjumbe wa makampuni ya China na wataalamu wa nchini na nchi za nje wameeleza matumaini yao kuwa nchi zao zitafanya ushirikiano zaidi wa kunufaishana.

    Mwezi Oktoba mwaka huu, kampuni ya teknolojia ya nishati mpya ya China BYD ilifanya sherehe ya kukamilishwa kwa ujenzi wa upanuzi wa kiwanda chake mjini Lancaster jimboni California nchini Marekani. Tangu mwaka 2013, kampuni ya BYD imewekeza dola za kimarekani milioni 230 katika soko la mabasi ya umeme nchini humo, na mabasi yake ya umeme yamechukua asilimia 80 ya mabasi yote ya aina hiyo yanayotumiwa nchini humo. Akizungumzia ziara hiyo ya rais Trump nchini China, meneja mkuu wa chapa na mahusiano ya umma ya kampuni hiyo Bw. Li Wei amesema anatarajia China na Marekani zitaimarisha ushirikiano katika sekta ya usafiri barabarani wa nishati mpya.

    "Nchi hizo mbili zinaweza kuongeza ushirikiano katika usafiri barabarani wa nishati mpya. Kabla ya kampuni ya BYD kuingia katika soko la Marekani, mabasi yake ya umma yanayotumia nishati mpya yalishaanza kutumiwa kwa miaka saba katika soko la China. Tuna takwimu nyingi za uendeshaji na uhifadhi, na mabasi yetu yanadumu sana. Kwanini mabasi yetu yanapendwa katika soko la Marekani, hii inatokana na kwamba yanaweza kutatua ukosefu wa teknolojia unaoikabili nchi hiyo."

    Balozi wa China nchini Marekani Cui Tiankai hivi karibuni alisema kama Marekani inaweza kulegeza masharti ya kuuza bidhaa zake za kiraia zenye teknolojia ya hali ya juu nchini China, itaweza kuongeza uuzaji bidhaa za Marekani kwa China, hii itasaidia kutatua suala la ukosefu wa uwiano katika biashara kati ya China na Marekani.

    Mwezi Agosti mwaka huu, Marekani ilianzisha uchunguzi wa kibiashara dhidi ya China katika sekta za makabidhiano ya teknolojia, hakimiliki na ubunifu, hatua ambayo imezua wasiwasi wa kuharibu uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Aliyekuwa mjumbe wa biashara wa Marekani Bibi Charlene Barshefsky amesema sera ya kujilinda kibiashara haikubaliki.

    "Naona China na Marekani zinabeba majukumu makubwa katika uongozi wa dunia, na zinapaswa kujenga uhusiano wa pande mbili wa kusaidiana na kunufaishana, na sera ya kujilinda ni adui wa pamoja wa nchi hizo mbili."

    Hivi sasa, uhusiano kati ya China na Marekani umezidi kuwa wa karibu, na ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Marekani pia umeingia kwenye kipindi kipya. Profesa Cui Fan kutoka Chuo Kikuu cha Uchumi na Biashara na Nje cha China anasema,

    "Kwa muda mrefu, suala la ukosefu wa uwiano katika biashara kati ya China na Marekani linasababishwa na sekta ya bidhaa na huduma. Naona katika siku za baadaye uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani utaangalia zaidi masuala ya mtaji, teknolojia na vipaji kutoka soko la bidhaa."

    Wataalamu wanaona kuwa ziara hiyo ya rais Trump nchini China itahimiza nchi hizo kufikia makubaliano mengi zaidi katika biashara ya pande mbili yenye haki na ya kunufaishana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako