• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu: Wachezaji watatu wa kikapu wa Marekani wakamatwa kwa wizi China

    (GMT+08:00) 2017-11-09 08:44:43

    Wachezaji watatu wa mpira wa kikapu wa ligi ya vyuo nchini Marekani wamekamatwa hapa China kwa wizi wa dukani. Wachezaji hao wa chuo kikuu cha California, mjini Los Angeles UCLA walikamatwa katika duka la Louis Vuitton. Klabu hiyo ya UCLA iko nchini kushiriki mechi ya ufunguzi wa ligi dhidi ya timu nyengine ya Marekani Georgia Tech.

    Wachezaji wanaoshikiliwa katika mji wa Hangzhou ni Cody Riley, LiAngelo Ball na Jalen Hill. Wanafunzi watatu wa Georgia pia walihojiwa lakini hawakukamatwa. Klabu hizo mbili ziko nchini ikiwa ni miongoni mwa malengo yao ya Pac-12 Global initiative ya kupija jeki uwepo wao na uzoefu wa kibinafsi wa wachezaji. Mechi hiyo ya kufungua msimu itakayochezwa kesho mjini Shanghai inafadhiliwa na Alibaba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako