• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza kuvaa vitambaa vyeusi katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Ujerumani

    (GMT+08:00) 2017-11-09 08:45:25

    Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza watavaa vitambaa vyeusi katika mchezo wao wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Ujerumani utakaochezwa kesho. Chama cha soka cha Uingereza kwa kushirikia na kile cha Ujerumani (DFB) vimethibitisha timu zote mbili kuvaa vitambaa hivyo kuungana na nchi hiyo katika kumbukumbu ya mashujaa waliokufa katika vita vya dunia. Mwezi Septemba Bodi ya Kimataifa ya Shirikisho la Soka (IFAB) ilitoa mamlaka kwa timu ya nyumbani kuvaa vitambaa vyeusi ikiwa ni ishara ya kumbukumbu ya tukio la heshima.

    Mkurugenzi wa chama cha soka nchini Uingereza, Martin Glenn amesema watatumia mchezo huo kwa kuvaa vitambaa kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa waliyoweza kuisadia nchi hiyo. Baada ya mchezo wa Ijumaa dhidi ya Ujerumani timu hiyo ya taifa ya Uingereza itashuka tena dimbani siku ya Jumatatu kuivaa Brazili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako