• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Russia asema vikwazo vilivyowekwa na Marekani havitaathiri ushirikiano wa teknolojia ya kijeshi na nchi za nje

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:00:58

    Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Russia Bw Viktor Bondarev amesema vikwazo vilivyowekwa na Marekani kwenye sekta za ulinzi na viwanda, havitaathiri ushirikiano wa teknolojia ya kijeshi kati ya Russia na nchi nyingine duniani.

    Bw Bondarev amesema ushirikiano wa teknolojia ya kijeshi na nchi nyingine utaendelea bila ya kijali vikwazo. Russia itaendelea kuboresha silaha, ili kuhakikisha uguvu yake ya ushindani kwenye soko la dunia. Russia itatoa kipaumbele kwa usalama wa kimataifa badala ya faida ya biashara.

    Wiki hii Rais Vladimir Putin wa Russia amesema thamani ya uuzaji wa silaha nje ya Russia katika mwaka huu, inatarajiwa kufikia dola bilioni 15.3 za kimarekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako