• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Syria yatangaza kusaini makubaliano ya Paris

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:08:14

    Kwenye duru mpya ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa Mataifa unaofanyika mjini Bonn, Ujerumani, wajumbe wa Syria wametangaza Syria itasaini na kujiunga na makubaliano ya Paris.

    Msemaji wa sekretarieti ya Mkataba wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa UNFCCC Bw. Nick Nutall, amethibitisha kuwa naibu waziri wa mazingira wa Syria Bw. Wadah Katmawi ameeleza kuwa Syria itasaini makubaliano hayo haraka iwezekanavyo.

    Bw. Nutall amesema Syria inatakiwa kukabidhi waraka wa serikali yake kuidhinisha kujiunga makubaliano ya Paris kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Mwezi Desemba mwaka 2015, nchi karibu 200 zilipitisha makubaliano kwenye mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa uliofanyika mjini Paris, lakini Syria ilikosa mkutano huo kutokana na mgororo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako