• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe asema atachukua hatua dhidi ya washirika wa aliyekuwa makamu wake

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:08:43

    Rais Rorbert Mugabe wa Zimbabwe amesema chama chake kitachukua hatua dhidi ya washirika wa aliyekuwa makamu wa Rais Bw Emmerson Mnangagwa, aliyefukuzwa kazi jumatatu.

    Rais Mugabe hakutaja hatua halisi zitakazochukuliwa dhidi ya washirika wa Bw Mnangagwa, lakini mikoa 10 ya chama chake jumanne imependekeza kuwa waungaji mkono wa Bw Mnangagwa pia watafukuzwa kazi.

    Washirika wa Bw Mnangagwa ni pamoja na waziri wa fedha wa zamani, ambaye ni waziri wa usalama wa mtandao wa Internet wa sasa Patrick Chinamasa, waziri wa usalama Bw Kembo Mohadi na waziri wa maji na mabadiliko ya hali ya hewa Oppah Muchinguri Kashiri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako