• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa ulinzi wa NATO wakubaliana kuanzisha idara mbili za uongozi wa kijeshi

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:34:50

    Mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa NATO wamekubaliana kuweka idara mbili mpya za uongozi wa kijeshi, ili kuongeza uwezo wa jumuiya hiyo wa kufanya uratibu wa vikosi na vifaa.

    Katibu mkuu wa NATO Bw. Jens Stoltenberg amesema hayo baada ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa nchi wanachama wa NATO uliofanyika katika makao makuu huko Brussels.

    Kati ya idara hizo mbili, moja itahakikisha usalama wa njia inayounganisha Amerika Kaskazini na Bara la Ulaya, nyingine itasaidia kuimarisha kusafiri kwa askar ndani ya bara la Ulaya..

    Bw. Stoltenberg pia ametoa wito kwa nchi wanachama kuboresha miundombinu na kuondoa vikwazo vya kimfumo, ili kuhakikisha majeshi ya jumuiya hiyo yanaweza kuvuka mipaka ya nchi bila matatizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako