• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ajali yaua watu 22 nchini Pakistani

    (GMT+08:00) 2017-11-09 09:37:54

    Takriban watu 22 wamefariki na wengine 51 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuangukia kwenye korongo usiku wa jana katika jimbo la Punjab nchini Pakistan.

    Taarifa za polisi wa eneo hilo zinasema kuwa watu 18 walifariki papo hapo na wengine wanne walifariki baadaye walipozidiwa na majeruhi, huku taarifa za madaktari zikiweka wazi kuwa huenda vifo vikaongezeka kufuatia hali za majeruhi wengine kuwa mbaya. Kwa mujibu wa taarifa za kipolisi, ajali hiyo ilisababishwa na mwendokasi uliomshinda dereva ambaye aliaminika kutokuwa na uzoefu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako