• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa China na Marekani wahudhuria ufungaji wa mazungumzo ya wenye viwanda wa nchi hizo mbili

  (GMT+08:00) 2017-11-09 18:22:27

  Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Donald Trump ambaye yuko ziarani nchini China wamehudhuria ufungaji wa mazungumzo ya wenye viwanda wa China na Marekani na kutoa hotuba.

  Rais Xi amesema, mwaka huu ni wa kuadhimisha miaka 45 ya Taarifa ya Shanghai iliyotolewa na China na Marekani. Katika miaka 45 iliyopita, uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili umetimiza maendeleo ya kihistoria, ambayo yamewanufaisha watu wa nchi hizo mbili. Hali halisi imeonesha kuwa nguvu za ushirikiano huo ni kubwa na zitanufaisha pande mbili kwa pamoja.

  Naye Rais Trump wa Marekani amesema, Marekani na China ni wenzi wa ushirikiano wenye uhusiano wa karibu, ambao wamefikia makubaliano mengi katika sekta za uchumi na usalama. Kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kutanufaisha maendeleo ya nchi hizo mbili.

  Habari zaidi zinasema, makampuni ya nchi hizo mbili leo yamesaini mikataba yenye thamani ya dola bilioni 250 za kimarekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako