• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la ndege la China Southern Airlines lashuhudia ongezeko la abiria wa Kenya

  (GMT+08:00) 2017-11-09 18:28:40

  Huu ni mwaka wa pili tangu shirika la ndege la China Southern Airlines kuzindua safari zake nchini Kenya. Shirika hili la ndege ambalo linaongoza katika ukanda wa Asia kwa usalama kwenye usafiri, una safari kwa zaidi ya maeneo 40, barani Afrika. Nchini Kenya, shirika hili limeshuhudia ongezeko la abiria wakenya na idadi hii inazidi kuongezeka.

  Ujio wa shirika la Ndege la China Southern Airline ulisaidia pakubwa kurahisisha usafiri wa moja kwa moja kutoka Kenya hadi China, hivyo kuwaokolea wasafiri wengi muda. Miaka miwili baada ya shirika hili kuanza shughughuli zake nchini Kenya, usafiri wake unazidi kuimarika kila kuchao. Wu Ve Jiing ni mkurugenzi mkuu wa shirka hilo hapa nchini Kenya.

  Kila kitu kiko sawa tangu tuzindue safari yetu ya kwanza ya ndege 5/8/2015. Baada ya safari hizi kuanza tulianza kushirikiana kwa karibu sana na wadau wa sekta ya usafiri wa ndege hapa nchini. Kwa sasa kuna safari ya moja kwa moja kutoka China hadi Nairobi. Hata hivyo, ushirikiano mwema kati yetu na shirika la ndege la Kenya Airways umetuwezesha kufikia vituo 44 kote Afrika. Marafiki zetu waafrika wanaoenda China, wanaweza kuunganishwa kwa mashirika mengine ya ndege bila tatizo lolote kwa sababu ya ushirikiano na uelewano mwema tulio nao na mashirika haya ya kimataifa. Wakitaka kuenda kwenye mataifa mengine kando na China, wataunganishwa bila wasiwasi katika mji wa Guangzhou.

  Kwa sasa, wakenya kati ya asilimia 20-30 wanatumia shirika hili la ndege kwa usafiri. Hata hivyo, changamoto kama vile joto la siasa ambalo limekuwepo hapa nchini liliathiri utendakazi wake pakubwa. Wu Ve Jiing anaeleza.

  Tunahitaji kuimarisha mauzo yetu. Wakenya wengi bado hawajui endapo tupo hapa nchini. Kinyume na mashirika mengine, sisi bado tunastahili kujitahidi sana kujiuza kwa wakenya na kuwafunza tamaduni zetu ili wakumbatie usafiri wa shirika hili letu. Hivyo basi lazima tuwe na uhusiano mwema nao.

  Shirika la China Southern Airlines limetoa ajira kwa vijana sita wa humu nchini kando na kuwapa mafunzo ya ziada.

  Tuna furaha sana kuwa miongoni mwa mwa wafanyikazi wa shirika hili tajika ulimwenguni…Kazi iko sawasawa…'

  Matarajio yao ni kwamba siku moja nao pia watapanda ngazi na kuwa mameneja kwenye shirika hili.

  'Tutafurahi sana kupiga hatua pia tuwe mameneja…

  Shirika hili linatarajia kutoa ajira zaidi kwa wakenya na hata kuimarisha maisha yao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako