Bw. Soumaila amesema hayo kwenye mkutano wa baraza la teknolojia ya habari na mawasiliano la Afrika, uliofanyika wakati wa maonyesho ya Mawasiliano ya Simu ya Afrika nchini Afrika Kusini. Amesema kuungana na internet kunaweza kubadilisha maisha ya watu katika sekta nyingi, ikiwemo afya, elimu, huduma za kifedha, kilimo, na kadhalika.
Kwa upande wake, mkuu wa kampuni ya Huawei eneo la Kusini mwa Afrika, Bw. Li Peng amesema watunga sera wa nchi nyingi za Afrika wameweka mazingira mazuri kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano, na kwamba makampuni yamefanya kazi muhimu katika kutoa teknolojia, ufumbuzi, huduma na mafunzo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |