• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa OCHA aonya kutokea kwa njaa kali Yemen visipoondolewa vizuizi

    (GMT+08:00) 2017-11-09 19:48:24

    Mkuu wa shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura la Umoja wa Mataifa OCHA Mark Lowcock ameonya kutokea kwa njaa kali nchini Yemen iwapo vizuizi vya anga, bahari na ardhini vilivyowekwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia havitaondolewa.

    Bw. Lowcock ametaka zichukuliwe hatua tano ili kuepusha balaa hilo la kibinadamu, zikiwemo kurejesha tena safari za ndege za Umoja wa Mataifa na washirika wake katika miji ya Sanaa na Aden nchini Yemen, kuhakikisha kuwa huduma za anga hazikatizwi, na makubaliano ya kuweka meli ya Mpango wa Chakula Duniani kwenye bahari ya Aden pamoja na kuhakikisha ufanyakaji kazi wake haukatizwi.

    Hatua nyingine ni upatikanaji wa vifaa vya kibinadamu na kibiashara kwenye bandari zote za Yemen, hususan vifaa vya lazima, na kuondoa vizuizi kwa meli zote zilizofuzu ukaguzi wa UN ili ziweze kufika kwenye bandari za Yemen haraka iwezekanavyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako