• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuandaa mkutano wa kimataifa wa tasnia ya filamu

    (GMT+08:00) 2017-11-09 19:49:02

    Ujumbe wa watu zaidi ya 100 unatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Filamu nchini Kenya wiki ijayo ili kutafuta njia za kutangaza na kuharakisha maendeleo ya tasnia ya filamu.

    Waziri wa Michezo, Utamaduni na Sanaa wa Kenya Hassan Wario amesema mkutano huo wenye kauli mbiu ya "kufikisha picha na sauti na tasnia ya filamu ya Afrika Mashariki kwenye kiwango kipya" utasaidia kujenga jukwaa kwa waigizaji wa kanda hiyo kubadilishana mawazo na kupanua mtandao na wenzao kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Wario amefafanua kuwa mkutano huo utapelekea maelewano mazuri ya kutumia fursa zilizopo kwenye tasnia hiyo kwa kuendeleza ushirikiano ili kuongeza sifa za pamoja.

    Mkutano huo utakaoanza tarehe 15 na kumalizika 17 ni juhudi za ushirikiano kati ya Bodi ya Filamu ya Kenya KFCB, Umoja wa Ulaya EU, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Matifa UNESCO na Ubalozi wa Ufaransa nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako