• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda:Kilimo cha Rwanda chakuwa kwa teknolojia

  (GMT+08:00) 2017-11-09 20:06:16

  Shirika la kilimo na huduma za dijitali limewapatia mafanikio makubwa wakulima nchini Rwanda kutokana na maelezo muhimu ya kuboresha kilimo chao.

  Kupitia kwa mtandao wa internet na application za zimu za rununu ,wakulima sasa wanaweza kufahamishwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa,kutakiwa kujiandaa na msimu wa mvua na kiangazi pamoja na kupewa ushauri wa kukabiliana na na changamoto.

  Mradio huu ulibuniwa na shirika la kimataifa la chakula FAO ,wizara ya kilimo na raslimali za wanyama na mifugo linalozingatia maendeleo ya kilimo nchini Rwanda.

  Wakulima wamekuwa wakipata hasara kubwa ya mali zao kutokana na kukosa ufahamu wa kilimo cha kisasa.

  Aidha shirika hilo limeanzisha mpango wa muwatafutia wakulima soko la bidhaa zao kwa bei bora.

  Idara ya utabiri wa hali hewa ya Rwanda inawasilisha maelezo ya kila siku kuhusiana na hali ya hewa kwa wakulima waliojisajili na tovuti hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako