• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Wavuvi wa pwani waingilia mauzo ya Tilapia

    (GMT+08:00) 2017-11-09 20:06:39

    Wavuvi katika mkoa wa pwani nchini Kenya wameingilia ufugaji na uuzaji wa samaki aina ya Tilapia ama mbuta katika mkoa wa Pwani ili kuongeza kipato.

    Watafiti wa shirika la viumbe vya baharini na samaki Kenya Marine and Fisheries Research Institute wamewashauri wavuvi kuingilia ufugaji huo ili kukabiliana na changamoto za uvuvi wa baharini.

    Mirera David mwanasayansi wa masuala ya viumbe vya majini anasema ufugaji huo una mapato makubwa ikilinganishwa na kutegemea bahari na msimu ya samaki.

    Mbali na hayo,soko la samaki wa Tilapia nchini Kenya limeongezeka pakubwa kutokana na mahitaji na sasa samaki aina hiyo hununuliwa hadi kutoka China na nchi za bara Asia.

    Wafugaji wanapata hadi shilinhi elfu 3,300 kwa mavuno ya awamu moja kwenye mita mraba wa 1200.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako