• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri mkuu wa China akutana na rais Trump

  (GMT+08:00) 2017-11-09 20:56:00

  Waziri mkuu wa China Li Keqiang leo hapa Beijing amekutana na rais Donald Trump wa Marekani.

  Kwenye mazungumzo yao, Bw. Li amesema hivi sasa uhusiano kati ya China na Marekani unaendelea vizuri, na ziara ya rais Trump nchini China itaingiza nguvu mpya ya uhai kwa pande hizo kuimarisha ushirikiano wao, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo ufikie kwenye kiwango kipya.

  Naye rais Trump ameeleza kuridhishwa na mafanikio yaliyopatikana kwenye ziara hiyo, na kutarajia nchi hizo mbili zitaimarisha ushirikiano, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, kuhimiza uhusiano wa kiuchumi na kibiashara wenye haki na uwiano, na kufanya uhusiano kati ya China na Marekani na ushirikiano wao kuendelezwa kwa nguvu zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako