• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • David Moyes asema anataka kujenga upya sifa yake katika klabu ya West Ham

  (GMT+08:00) 2017-11-10 09:13:58

  Meneja mpya wa West Ham David Moyes amesema anataka kutuma ujumbe na pia kujenga upya sifa yake katika klabu hiyo. Meneja huyo wa zamani wa Everton na Manchester United alichukua nafasi ya Slaven Bilic, aliyetimuliwa Jumatatu klabu hiyo ikiwa eneo la kushushwa daraja kwenye jedwali. Moyes, 54, amekuwa hana kazi tangu Mei alipojiuzulu wadhifa wake kama meneja wa Sunderland baada ya klabu hiyo kushushwa daraja. Meneja huyo ambaye alianza kazi yake Preston North End, alishinda tuzo ya Meneja wa Mwaka wa LMA mara tatu akiwa Everton kati ya 2002 na 2013. West Ham wapo nafasi ya 18, baada ya kushinda mechi mbili pekee Ligi ya Premia msimu huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako