• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sergio Aguero ana mpango wa kuacha soka ya kimataifa

  (GMT+08:00) 2017-11-10 09:14:43

  Straika wa Manchester City na timu ya taifa ya Argentinian, Sergio Aguero amesema wakati mkataba wake utakapomalizika mwaka 2019 atarejea kuitumikia klabu yake ya zamani ya Independiente ya nchini kwao. Katika kipindi hiki cha miaka sita alichoitumikia Manchester, Aguero amefanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Eric Brook kwakuwa mfungaji wa muda wote baada ya kutupia bao safi katika mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Napoli. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atarejea katika klabu yake ya utotoni ya Independiente wakati atakapo maliza mkataba wake wa miaka wili Etihad huku akisisitiza kuwa hilo ndilo wazo lake. Aguero kwa sasa yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya Argentina ambayo inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Urusi na Nigeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako