• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya magongo ya Kenya Rodgers Ayuya, afariki dunia

  (GMT+08:00) 2017-11-10 09:15:02

  Nyota wa zamani wa timu ya taifa ya magongo ya Kenya, Rodgers Ayuya, amefariki dunia. Ayuya alifariki juzi Jumatano baada ya kupata ajali mbaya ya barabarani alipokuwa akiendesha lori lililopoteza mwelekeo na kugonga mti kwenye barabara ya Bungoma-Mumias. Katika enzi za uhai wake, alikuwa mshambuliaji hodari. Marehemu Ayuya alihamia klabu ya Wazalendo na kisha Greensharks ambayo aliichezea kutoka mwaka 2006 hadi 2011 kabla ya kuungana na Lugalia tena katika klabu ya Western Jaguars. Alichezea Kenya kati ya mwaka 2005 na 2008.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako