• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Ulaya na nchi za Kiarabu wataka kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za pamoja

    (GMT+08:00) 2017-11-10 09:18:03

    Viongozi wa nchi za Ulaya na nchi za Kiarabu wanaohudhuria kongamano kati pande hizo mbili linalofanyika huko Athens, Ugiriki kwa lengo la kujenga daraja la mazungumzo na ushirikiano kati ya nchi hizo, wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto za pamoja na kutimiza maendeleo na ustawi wa nchi zote.

    Waziri mkuu wa Ugiriki Bw. Alexis Tsipras amesema kutokana na sababu za kisiasa, kijiografia na kihistoria, Ugiriki ni daraja la mawasiliano kati ya Ulaya na nchi za kiarabu.

    Naibu mkuu wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mambo ya nishati Bw. Maros Sefcovic amesema pande mbili zinatakiwa kufanya mazungumzo kwa sababu Umoja wa Ulaya na nchi za Kiarabu zina maslahi mengi ya pamoja, nchi nyingi ni jirani, na zina changamoto na fursa za pamoja katika mambo ya usalama, ugaidi, uhamiaji haramu, mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo ya uchumi na biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako