• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Masumbwi: Deontay Wilder asisitiza kuwa yupo tayari kuzitwanga na Anthony Joshua

  (GMT+08:00) 2017-11-10 09:27:03

  Bondia wa uzito wa juu nchini Marekani, Deontay Wilder amesisitiza kuwa yupo tayari kupigana na bingwa wa dunia wa uzito wa juu Muingereza, Anthony Joshua na kamwe hawezi kuipoteza nafasi hiyo hadhimu. Kupitia mahojiano yake na Sky Sports meneja wa Joshua, amesema wanataanza kufanya mazungumzo na bondia Wilder ili kufikia muafaka wa pambano hilo. Wakati bingwa huyo wa WCB, Wilder amethibitisha kuanza kufanyika kwa mazungumzo hayo lakini amemtaka mfalme wa IBF na WBA, Anthony Joshua kutokufanya maamuzi mengine kabla ya kikao chao kilichopendekezwa. Wilder amecheza mapigano 39 bila kupigwa hata moja huku mwishoni mwa wiki iliyopita alifanikiwa kutetea mkanda wake wa WBC dhidi ya Bermane Stiverne.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako