• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yazidi kuwashukia viongozi wa Catalunya

    (GMT+08:00) 2017-11-10 09:59:21

    Mjini Madrid, Mwendesha mashtaka mkuu wa serikali ya Hispania amependekeza vifungo vya muda usiojulikana dhidi ya viongozi wanne wa serikali ya jimbo la Catalunya. Taarifa hiyo inaeleza kuwa spika wa zamani wa bunge la Catalunya Carme Forcadell alihojiwa jana pamoja na viongozi wengine watano wakidaiwa kuasi, uchochezi na matumizi mabaya ya fedha.

    Bunge la Catalunya lilijitangazia uhuru wa jimbo lake Oktoba 27, jambo ambalo hata hivyo lilipingwa na kubatilishwa na serikali ya Hispania na kufanya baadhi ya viongozi wa jimbo hilo kufungwa isipokuwa Rais wa zamani wa Catalunya Carles Puigdemont ambaye yuko nchini Ubelgiji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako