• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping amewasili Vietnam kwa ajili ya ziara rasmi na mkutano wa APEC

    (GMT+08:00) 2017-11-10 18:01:34

    Rais Xi Jinping wa China amewasili huko Da Nang, nchini Vietnam kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Nchi za Asia na Pasifiki APEC na kufanya ziara rasmi nchini Vietnam.

    Rais Xi Jinping anatarajiwa kutoa hotuba kwenye mkutano wa wakuu wa makampuni wa nchi za APEC, na kuhudhuria mazungumzo ya baraza la washauri wa biashara, pamoja na mazungumzo yasiyo rasmi na viongozi wa jumuiya ya nchi za Asia kusini, pia anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na viongozi wa nchi nyingine wanaohudhuria mkutano wa APEC.

    Hii ni ziara ya kwanza kwa rais Xi Jinping nje ya nchi, tangu mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti cha China ufungwe.

    Baada ya kuhudhuria mkutano wa APEC unaofanyika leo na kesho, Rais Xi atafanya ziara nchini Vietnam na Laos kati ya Novemba 12 na 14.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako