• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli aahidi kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje

    (GMT+08:00) 2017-11-10 18:46:21

    Rais John Pombe Magufuli ameahidi kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje kama viwanda vya sukari nchini humo vitazalisha sukari ya kutosha ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani. Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha sukari mkoani Kagera, Magufuli amesema mahitaji ya sukari nchini Tanzania ni tani 450, 000 lakini uwezo wa kuzalisha wa viwanda vyote kwa jumla ni tani 320,000 na hivyo kusababisha upungufu wa tani 130,000.

    Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa mkoani Morogoro kina uwezo wa kuzalisha tani 30,000, Kiwanda cha Sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro tani 100,000, Kiwanda cha Sukari cha Kilombero mkoani Morogoro tani 109,000, Kiwanda cha Sukari mkoani Manyara tani 6,000, Kiwanda cha sukari cha Kagera tani 65,000 hadi tani 67,000 ingawa kwa mwakani kimepanga kuzalisha tani 75,000.

    Magufuli ameongeza kuwa viwanda vingine vinajengwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF ambavyo vitaongeza uzalishaji wa sukari nchini. Aidha, Rais aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kujenga viwanda vya sukari kwa kadri ya uwezo walionao kwa kuwa soko la bidhaa hiyo ni kubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako