• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya yaitaka NCPB kuondoa ada ya kukausha nafaka

    (GMT+08:00) 2017-11-10 18:47:25

    Waziri wa kilimo wa Kenya Bw Willy Bett ameitaka bodi ya kitaifa ya nafaka NCPB kuondoa ada ya kukausha nafaka ili kuepushia wakulima hasara.Waziri huyo amesema wakulima wanaweza kupata hasara ya hadi asilimia 20 baada ya kuvuna kwa sababu ya mvua inayozidi kushuhudiwa katika maeneo tofauti nchini Kenya. Amesema serikali itagharamia ada hizo.Hata hivyo Bett amesema hiyo ni kwa wakulima ambao watapeleka mazapo yao kwa NCPB pekee wala si wale wanaotaka kwenda kukaushiwa kisha waondoke na nafaka zao.Amesema hivi sasa wanapokea kiwango kidogo cha nafaka kwasababu ya mvua.Wakati huo huo bodi hiyo imesema mazao ya wakulima yana unyevu unaofika asilimia 20 ilhaliwanakubali tu kiwango cha asilimia 18 kiwandani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako