• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yataka ujenzi wa bomba la mafuta kukamilika kabla ya 2020

  (GMT+08:00) 2017-11-10 18:49:19

  Rais John Pombe Magufuli ametaka ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ukamilike mapema kabla ya mwaka 2020 ili uzalishaji wa mafuta uanze.

  Akizungumza nchini Uganda, amesema hakuna sababu ya kuchukua muda mrefu kwa sababu mkandarasi anaweza kufanya kazi kwa saa 24, lakini pia kazi hiyo inaweza kugawanywa kwa wakandarasi 10 kila mmoja ajenge kilomita 145.

  Kauli hiyo aliitoa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo. Jiwe hilo liliwekwa kwenye kijiji cha Luzinga, mkoa wa Rakia nchini Uganda baada ya uzinduzi kama huo kufanyika kwanza Chongoleani, mkoani Tanga, Agosti 05, mwaka huu.

  Bomba hilo litajengwa na kuendeshwa na Kampuni ya Bomba la Mafuta kwa ubia na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Uganda (NOC), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni tatu za mafuta za CNOOC, TOTAL na TULLOW kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 3.5.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako