• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuondoa vizuizi dhidi ya wawekezaji wa kigeni

  (GMT+08:00) 2017-11-10 19:33:17

  China imetaja hatua itakazochukua ambazo zitapunguza au kuondoa vizuizi vya uwekezaji wa kigeni kwenye masoko yake ya mitaji.

  Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari, Naibu Waziri wa Fedha wa China, Bw. Zhu Guangyao amesema kuwa sasa wafanyabiashara wa kigeni wataruhusiwa kumiliki hadi asilimia 51 ya hisa kwenye ubia wa dhamana, fedha, na malipo ya baadaye.

  Akifafanua kuhusu makubaliano yaliyofikiwa kati ya China na Marekani katika mkutano wa jana, Bw. Zhu amesema, China itaondoa masharti yote ya uwekezaji kwenye mabenki yake na hata katika taasisi nyingine za kifedha .Kwa upande wa Marekani imeombwa kutimiza mambo mbalimbali ikiwemo kupunguza udhibiti wa usafirishaji wa bidhaa za teknolojia ya juu, kutimiza wajibu wake chini ya kifungu cha 15 cha Mkataba wa China kujiunga na Shirika la Biashara Duniani WTO na kuwatendea haki wawekezaji wa China nchini Marekani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako