• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Saudi Arabia na Qatar zawataka raia wao kuondoka Lebanon haraka iwezekanavyo

    (GMT+08:00) 2017-11-10 19:33:40

    Wizara za mambo ya nje za Saudi Arabia na Qatar zimetoa taarifa kwa nyakati tofauti zikiwataka raia wao walio nchini Lebanon waondoke nchini humo haraka iwezekanavyo, na wengine wasiende nchini humo hivi karibuni.

    Kabla ya hapo, Bahrain nayo ilitoa onyo la kutosafiri kwa raia wake nchini Lebanon .

    Tarehe 4 mwezi huu, waziri mkuu wa Lebanon Bw. Saad Hariri alitangaza kujiuzulu, huku akiilaani Iran kwa kuingilia mambo ya ndani ya Lebanon na nchi nyingine za kiarabu kupitia kuunga mkono kundi la Hezbollah. Pia amesema, maisha yake yako hatarini.

    Naye Rais Hassan Rouhani wa Iran alijibu lawama hizo akisema hazina msingi wowote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako