• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China ahutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa APEC

    (GMT+08:00) 2017-11-11 17:18:09

    Rais Xi Jinping wa China jana amehudhuria na kuhutubia mkutano wa kilele wa viongozi wa viwanda na biashara wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Uchumi wa Nchi za Asia na Pasifiki APEC, akisisitiza kuwa dunia inabadilika kwa kasi, huku uchumi wa dunia ukibadilika kwa kina zaidi, nchi wanachama wa APEC zinapaswa kubeba majukumu ya kuanzisha mustakabali mzuri wa sehemu ya Asia na Pasifiki.

    Rais Xi ametoa mapendekezo manne ya kuendelea kujenga uchumi wa kufungua mlango na kujitahidi kunufaishana na kupata mafanikio ya pamoja, kuendelea kujitahidi kupata ongezeko la uvumbuzi na kutafuta injini mpya za maendeleo, kuendelea kuimarisha mawasiliano na muungano ili kupata maendeleo ya pamoja, na kuendelea kuongeza uvumilivu wa maendeleo ya uchumi ili kuwanufaisha watu wote.

    Rais Xi amesisitiza kuwa ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, China inajua majukumu yake, na katika miaka mitano iliyopita imedumisha ongezeko la uchumi na kuendelea kuwa injini ya maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako