• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na viongozi wa Japan na Korea ya Kusini

    (GMT+08:00) 2017-11-12 16:22:22

    Rais Xi Jinping wa China jana huko Da Nang, Vietnam kwa nyakati tofauti amekutana na viongozi wa Japan na Korea ya Kusini.

    Alipokutana na waziri mkuu wa Japan Bw. Abe Shinzo rais Xi amesema, huu ni mwaka wa 45 tangu China na Japan zirejeshe uhusiano wa kawaida, nchi hizo mbili zinapaswa kuzingatia maslahi ya wananchi wao, kushikilia mwelekeo wa amani, urafiki na ushirikiano, na kujitahidi kuboresha zaidi uhusiano kati yao.

    Alipokutana na rais Moon Jae-in wa Korea ya Kusini, rais Xi amesema China na Korea ya Kusini ni majirani wasiohamika na wenzi wa ushirikiano. Uhusiano mzuri kati ya nchi hizo mbili unafuata hali ya historia na zama za kisasa, pia ni matumaini ya pamoja ya wananchi wa nchi hizo mbili. China inatilia maanani uhusiano kati yake na Korea ya Kusini, na kupenda kushirikiana na Korea ya Kusini kusukuma mbele uhusiano huo kuendelea vizuri na kwa utulivu.

    rais Xi siku hiyo pia amekutana na rais Rodrigo Duterte wa Philippines.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako