• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa Marekani na Russia wasisitiza kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2017-11-12 17:51:04

    Rais Donald Trump wa Marekani na rais Vladimir Putin wa Russia jana Jumamosi walifanya mazungumzo katika kipindi cha mkutano usio rasmi wa viongozi wa jumuiya ya APEC, pande hizo mbili zilisisitiza kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa.

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa tangazo la pamoja lililotolewa na pande hizo mbili. Tangazo hilo lilisema kuwa, pande hizo mbili zilifikia makubaliano kuwa hazitachagua njia ya kijeshi kwa kutatua mgogoro wa Syria, ni lazima kutekeleza azimio la nambari 2254 la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na kupanga mpango wa utatuzi wa kisiasa kwenye msingi wa mchakato wa Geneva. Marais hao wawili walizitaka pande zote za Syria zifanye juhudi kujiunga na mchakato huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako