• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa mwito wa kuhimiza uhusiano kati ya China na Vietnam

    (GMT+08:00) 2017-11-13 09:15:42

    Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito wa kuhimiza uhusiano wa pande zote na wa kimkakati kati ya China na Vietnam, na kuendelea kuwa majirani wema, marafiki wakubwa na washirika wazuri.

    Rais Xi amesema ziara yake nchini Vietnam ina lengo la kuhimiza urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili, kuimarisha ushirikiano na kuweka mipango ya ushirikiano wa pande mbili katika siku za baadaye.

    Rais Xi amesema kutokana na kuwa China na Vietnam zote ni nchi zinazoongozwa na vyama vya kikomunisti na zinafuata njia ya ujamaa, zinaimarisha umoja na ushirikiano, kwa ajili ya maslahi ya kimsingi ya watu wake na amani, utulivu na maendeleo ya kikanda na dunia.

    Rais Nguyen Phu Trong amesema anaamini kuwa ziara ya Rais Xi nchini Vietnam itahimiza uhusiano wa pande mbili, na nchi yake iko tayari kuhimiza ushirikiano na China kuwa endelevu, wenye nguvu na wa kimkakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako