• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Lebanon athibitisha kurejea Lebanon katika siku chache zijazo

    (GMT+08:00) 2017-11-13 09:19:19

    Waziri mkuu wa Lebanon Bw Saad Hariri amethibitisha kuwa atarejea Beirut katika siku chache zijazo.

    Bw Hariri ameonekana kwa mara ya kwanza kwenye televisheni tangu ajiuzulu ghafla Novemba 4 wakati akihojiwa na televisheni moja ya Saudi Arabia. Amesema kabla ya kujizulu alijadili hatari zinazoikabili Lebanon vikiwemo vikwazo vya Marekani na nchi za Kiarabu. Kuhusu makubaliano ya kisiasa aliyofikia, amesema ili yaendelee wanatakiwa kujitenga na masuala ya kikanda na kwamba Walebanon hawapaswi kuathirika baada ya kundi la Hezbollah kujihusisha na mgogoro wa Syria wa kuulinda utawala wa rais Bashar Assad, na shutuma za Saudi Arabia dhidi ya kundi hilo kujihusisha na migogoro nchini Yemen, Bahrain na Iraq.

    Hata hivyo Lebanon inaona kujiuzulu kwa Hariri kunatokana na kulazimishwa na Saudi Arabia. Rais wa nchi hiyo Michael Aoun alisema tangazo lolote la kujiuzulu lililotolewa na Hariri kutoka Riyadh linaibua wasiwasi. Lakini Hariri amedai kuwa yuko huru nchini Saudi Arabia na hakulazimishwa kujiuzulu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako