• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tunisia na Misri zataka kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na kiuchumi

  (GMT+08:00) 2017-11-13 09:31:49

  Waziri mkuu wa Tunisia Bw. Youssef Chahed ametoa taarifa mjini Cairo akisema, Tunisia inapenda kuimarisha ushirkiano wa kiusalama, kiuchumi na kibiashara na Misri.

  Bw. Chahed amesema hayo baada ya kukutana na rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri, kabla ya kuhudhuria kongamano la 16 la kamati ya juu ya pamoja ya Misri na Tunisia akiwa pamoja na mwenzake wa nchi hiyo Bw. Sherif Ismail.

  Bw. Chahed amesema Tunisia inapenda kuimarisha ushirikiano wa kiusalama na Misri kupitia kamati ya pamoja inayopanga kukutana mwezi huo kujadili juhudi za pamoja katika mapambano dhidi ya ugaidi.

  Nchi jirani za kiarabu zikiwemo Libya, Misri, Tunisia na Algeria zimeratibu misimamo yao na kuhimiza mazungumzo kati ya pande zinazopambana nchini Libya ili kufikia utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako