• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Kenyatta wa Kenya atetea ushindi wake katika uchaguzi wa marudio

  (GMT+08:00) 2017-11-13 09:32:29

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametetea ushindi wake katika uchaguzi wa urais uliorudiwa, huku akisema upigaji kura uliofanyika Oktoba 26 umefuata katiba na sheria.

  Rais Kenyatta akijibu maombi ya pingamizi la uchaguzi amesema licha ya kutokea kwa vurugu katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo hasa katika sehemu ambazo ni ngome ya chama cha upinzani cha NASA, uchaguzi huo ulifikia vigezo vya kikatiba na kisheria vya uchaguzi wa kuaminika, huru na wenye usawa.

  Pia ametaka mapingamizi yaliyotolewa na wanasiasa yaondolewe, huku akiongeza kuwa watu hao hawana madai ya ukweli yanayoweza kufuta matokeo ya uchaguzi huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako