• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa Umoja wa Mataifa na waziri mkuu wa Libya wajadiliana kuhusu maendeleo ya hali ya kisiasa

  (GMT+08:00) 2017-11-13 09:41:39

  Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Libya Bw. Ghassan Salame, jana alikutana waziri mkuu wa Libya anayeungwa mkono na Umoja wa Mataifa Bw. Fayez Serraj huko Tripoli, kujadili ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo.

  Kwa mujibu wa ofisi ya vyombo vya habari ya waziri mkuu wa Libya, mkutano huo umejadili maendeleo yaliyopatikana hivi karibuni katika hatua ya utatuzi wa kisiasa wa mgogoro nchini humo, na mipango ya kipindi kijacho iliyopendekezwa na Bw. Salame, ambayo itaelekeza uchaguzi wa rais na wabunge wa nchi hiyo.

  Bw. Salame atahutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya hali ya kisiasa nchini Libya Novemba 16.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako